Tuesday, November 13, 2012

KUWEKEA NDOA YAKO MSINGI MZURI




KUWEKEA NDOA YAKO MSINGI MZURI
Nyumba , maisha au ndoa inakuwa nzuri ikiwa msingi wake ni mzuri tu. Katika mmojawapo wa mifano yake, Yesu alisema habari ya watu wawili-mtu mwenye akili aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba mgumu na mtu mpumbavu aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga. Upepo mkubwa ulipotokea, mafuriko(maji) na pepo zikapiga nyumba hizo mbili. Ile iliypjengwa juu ya mwamba mgumu ilibaki ikisimama, lakini ile iliyojengwa juu ya mchanga ilianguka kwa anguko kubwa.
                Yesu hakuwa akiwafundisha watu namna ya kujenga nyumba. Alikuwa akikazia uhitaji(lazima) wa kuweka maisha juu ya msingi nzuri. Akiwa mjumbe wa Mungu alisema hivi: “Kila asikiaye hayo maneno yangu na kuyafanya”, anafanana na mtu anayejenga juu ya mwamba. Lakini “kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye,” anafanana na Yule anayejenga juu ya mchanga. –Mathayo 7:24-27
                Fahamu kwamba katika mifano hiyo miwili Yesu anaonyesha kwamba si kusikia tu shauri la hekima na kujua tu jambo la kufanya. Kinachotofautisha kufanikiwa na kushindwa ni kufanya shauri la hekima linavyosema. “Mkiyajua hayo, (wenye furahani) ninyi mkiyatenda.” – Yohana 13:17.
                Hivyo ndivyo ndoa ilivyo. Tukiweka ndoa yetu juu ya msingi ulio kama mwamba, itashinda mikazo ya maisha. Lakini msingi huo ulio mzuri unatoka wapi? Kwa muumba wa ndoa, Yehova Mungu.Yeye alianza ndoa alipowaunganisha watu wawili wa kwanza wawe mume na mke. Kisha akawapa maagizo ya hekima ili wapate faida. Jambo ambalo lingeamua kama wangeishi milele ama sivyo, lingetegemea kufuata maagizo hayo. Wote wawili waliyajua maagizo ya Mungu, lakini jambo la kusikitisha ni kwamba waliruhusu choyo kiwazuie wasitii maongozi hayo. Walichagua kutokufuata shauri hilo na, kwa sababu hiyo, ndoa na maisha yao yaliharibika kama nyumba iliyojengwa juu ya mchanga.
                Yehova Mungu aliwaunganisha watu wawili wa kwanza katika ndoa, lakini yeye mwenyewe hawafanyii watu waliooana mipango ya ndoa leo. Walakini, shauri lake juu ya ndoa lingali linapatikana. Ni juu ya kila mtu leo anayejifikiria kuoa au kuolewa aamue kama atafuata shauri hilo au hatalifuata. Vilevile neno la Mungu linaonyesha kwamba tunaweza kumwomba atusaidie tuamue kwa hekima juu ya mtu tunayetazamia kuoana naye. –Yakobo 1:5,6
                Walakini, hali zinatofautiana sana katika sehemu mbalimbali za dunia.Leo katika sehemu nyingi za  dunia, wanaume na wanawakewanajichagulia wenyewe mtu wa kuoana naye. Lakini katika sehemu ya watu wanaoishi duniani leo, watu wengi leo hujichagulia mabinti na vijana wa kuwaoa au kuolewa nao tena hukutana nao Vyuoni, maofisini na hata barabarani. Katika sehemu nyingi za dunia kijana anapata mke mara baada ya kulipishwa mahari tena kubwa jambo ambalo sina hakika kama ni mpango wa Mungu, Ndipo kijana ujikakamua na tena kwa sononeko moyoni ambalo baadae uja kuzaa manyanyaso kwa binti. Lakini hata hali ziwe namna gani, Biblia imetoa shauri linaloweza kusaidia ndoa ifanikiwe kwa muda mrefu.