Monday, October 22, 2012

KUFAHAMIANA TABIA NA KUZIFURAHIA TOFAUTI HIZO KUTADUMISHA FAMILIA.

Kufahamiana kwa tabia kwa mume au mke alivyo hasa kutasaidia kukuza familia yenye furaha na kurekebisha yasiyofaa.Kufuatisha wataalamu wa saikolojia kama vile Robert Cruise na Peter Blitchington wa chuo kikuu cha Andrews na wengineo palitokea uamsho wenye mvuto mkubwa katika miaka ya 1990’s kuhusiana na mada hii. Ilionekana kuwa wanadamu wamegawanyika katika tabia/mwenendo aina kuu 4, ili uweze kugundua mmeo au mkeo ana aina ipi na muweze kuungana na kuwa mwili mmoja. Soma Mwanzo 2:24.
1.Choleric
a)Kihisia. Anajiamini katika uamuzi wake, Ana nia thabiti, Mgumu, Shupavu, Aaminiye kuwa yote yatatokea vizuri, Haogopi kitu, Macho makavu, Mkali sana, Ana hasira kiasi cha kutumia nguvu, Hapendezwi kulia lia.
b)Uhusiano na wengine.
Hatazamii mwingine kufanya asichokiweza, Hakati tamaa upesi, Kiongozi mwenye bidii, Mwamuzi mzuri, Mhamasishaji wa mambo, Mshauri, Hatishwi na mazingira, Hana huruma, Huamua mahali pa wengine, Aweza kuwa mkatili, Msema wazi bila kusifu sifu, Aweza kutia uchungu, Huelekea kuwa na amri juu ya ….., Mwene kudeka, Bwana, Mtumia watu kwa faida yake, Asiyesamehe, Mlipiza kisasi, Shupavu, Mwenye dharau.
c)Kazi.
Mpangaji na mkuzaji mzuri, Kauli bora, Mwepesi na hodari, Mchapa kazi, Uwezo mkubwa wa utendaji, Hasitisiti, Huwatia nguvu wengine kufanya kazi, Hukabili upinzani, Huweka malengo na kuyafikia, Hupenda ajenda, Anajiamini sana, Mwerevu, Mshika shauri lake, Huwalazimisha wengine kufuata yake, Hawasiliani na wengine juu ya ajenda zake, Mgumu kupendeza, Huchosha, Huvunjika moyo mambo yasipokamilika.
2.Melancholy.
a)Kihisia
Mpenda muziki na sanaa, Mchanganuzi, Mwepesi kuona, Kukasirika, Kutovumilia hali, Mwenye kufikiria mambo kwa kina, Hufurahia usanifu, Huhurumia, Mwenye moyo mzito, Hutazama sana upande wa hasi, Hupenda kuteseka, Mfia dini, Mwenye mashaka juu ya afya, Mwenye kujiwazia, Mwenye huzuni, Hujivuna.
b)Uhusiano na wengine
Rafiki wa kutumainia, Hujitolea mhanga, Mwaminifu, Hufanya urafiki kwa hadhari, Husahau mambo, Huwafikiria sana wengine, Mjenzi wa mapokeo ya kifamilia, Msikilizaji mzuri, Hukosoa sana mapungufu ya wengine, Hutaka ukamilifu na huamua kila kitu kwa mtazamo wake, Huhofia yale
wamfikiliayo wengine, Haamini wengine, Aweza kutumia nguvu hasira iliyoendelezwa kuleta uadui, Huumizwa na mambo ya wengine, Anaweza kufunga fundo la ugomvi wa kale na kulipiza, Hawapendi wanaompinga.
c)Kazi
Mpenda ukamilifu, Hupenda kazi yote ni mwenye nidhamu, Hukamilisha alichonuia, Mbunifu, Mwenye busara na akili, Ajua mipaka yake, Si dhahiri mpenda nadharia, Hachoki upesi, Husita kuanza mradi mpya, Wachanganuzi mno, Humwongoza kukata tama, Hufurahia uumbaji.
3.Phlegmatic
a)Kihisia
Mtulivu,Hutumainika, Hajiamini, Kuchukuliana, Hasadiki hivi hivi, Mwoga, Mwepesi kufadhaika, Mkunjufu hata kama hana neno, Mwenye huruma mpenda amani, Hukubali kupatana.
b)Uhusiano na wengine
Huffurahia kuwa naye ana rafiki wengi, Mwana diplomasia, Mpatanishi, Msikilizaji, Rafiki mwaminifu, Hutoa ushauri anapoombwa, Mchekeshaji, Mnyimifu, Mtundu, Ni baridi kwa wengine huwanyanyasa au kuwachambua wanaomsumbua, Hakaribishi vizuri, Hujiona mkubwa.
c)Kazi
Hufanya kazi vizuri kwa msukumo, Mtulivu, Mwenda pole, Mvivu, Hapendi mabadiliko, Msafi na mwelekevu, Hupanga kazi kabla ya kuianza, Hukatisha tamaa ubunifu wa wengine.
4.Sanguine
a)Kihisia
Mkunjufu sana, Mcheshi, Msemaji sana hajali yaliyopita wala yajayo, Mpenda hadithi, Huishi kwa yaliyopo mpenda raha, Ana kelele, Hajitawali, Huamua na kununua kwa urahisi bila shauri, Ana tabia za kitoto, Hutokea kwa mshindo.
b)Uhusiano na wengine
Hujipatia marafiki haraka, Hufurahisha, Daima hufurahisha na ni rafiki, Mwepesi kuomba radhi, Huhurumia, Huongea kwa uchangamfu wa kweli, Hushiriki furaha na masikitiko yaw engine, Hutaka azungumze yeye tu hata bila kufikiri vizuri, Si msikivu, Nia hafifu, Hutafuta sifa na kukubalika, Huwafurahia watu na kuwasahau, Huongelea sana juu ya nafsi yake, Husahau ahadi na wajibu.
c)Kazi
Hana mpangilio lakini ana mvuto kwa mara ya kwanza, Si wa kuamini, Mchelewaji, Hana nidhamu hupoteza muda, Kazi zake nyingi hazikamiliki, Mwenye wasi wasi, Hafikii lengoHuingilia mipango mipya kwa urahisi, Ana talanta ya kutunza wagonjwa.

Ukijua mumeo/mkeo ni aina ya
a)Choleric au
b)Melancholy au
c)Phlegmatic au
d)Sanguine ni njia ipi ungeitumia kuwafanya muishi pamoja kwa amani?
I)Kumnunia, kumkosoa tabia yake, avaavyo, afanyavyo mambo kwa sababu yeye hajali haoni kuwa mimi sipendi mambo yake. NI KUMPASHA UKWELI WAKE.
II)Ukijua udhaifu wa wenzako tena mkiwa ndani ya ndoa jitahidi kumjibu kwa upole, Mithali 15:1. Mpende na kumtia moyo mfurahie alivyo maana yeye ndiye mumeo/mkeo. Umsifu kwa yale mazuri aliyo nayo , pia mvumilie.
“Tunatofautiana sana katika silica, tabia, elimu, kiasi kwamba namna tunavyoyatazama mambo hutofautiana. Huamua namna tofauti. Namna ya kuelewa kwetu ukweli, mawazo yetu kuhusiana na mambo ya maisha hutofautiana sana. Hapana watu wawili wanaofanana kabisa mambo yao ya maisha katika kila jambo. Majawabu ya huyu si majaribu ya Yule. Wajibu ambao mmoja anao ni mwepesi ni mgumu na wa kutatiza kwa kwa mwingine” GW 473. Kumwelewa mwenzako alivyo kutasaidia kukuza uhusiano na umoja wenu.

No comments:

Post a Comment