Asilimia 26.5 wanawake hufanya mapenzi kinyume na maumbile
Na Florence Majani
Wakati idadi ya wanawake wenye maambukizi ya Virusi
vya Ukimwi ikiongezeka, asilimia 26.5 ya wanawake Tanzania wamebainika
kuwa wanafanya mapenzi kinyume na maumbile.
Wakati idadi ya wanawake wenye maambukizi
ya Virusi vya Ukimwi ikiongezeka, asilimia 26.5 ya wanawake Tanzania
wamebainika kuwa wanafanya mapenzi kinyume na maumbile.
Mfumo wa uzazi unaharibika
Watafiti wanabainisha kuwa kitendo hicho licha ya
ukweli hakifai kwa vile kinaharibu mfumo wa uzazi, kina athari kubwa mno
kwa mwanadamu, mojawapo ni ikiwemo uwezekano mkubwa wa wahusika
kuambukizana virusi vya Ukimwi kwa vile hakuna vilainishi, hivyo
kusababisha michubuko ambayo ndio njia kuu ya kuambukiza vijidudu hivyo.
Mtafiti Mwanasayansi, Irene Mremi kutoka Taasisi
ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu nchini Tanzania (NIMR)
alitoa ripoti hiyo hivi karibuni hapa jijini Dar Es Salaam.
Mremi akiwa na jopo la watafiti kutoka NIMR
anasema kuwa wanawake hao wamesema chanzo kikubwa kinacho wapelekea
kufanya ngono kinyume na maumbile ni kujipatia kipato zaidi na Kuogopa
kupata Mimba.
Vilevile alizitaja sababu nyingine za wanawake
kufanya mapenzi kwa njia hiyo ni kulinda usichana wao na baadhi ya mila
na tamaduni za baadhi ya makabila.
Sampuli za utafiti
Utafiti huo ulikusanya sampuli kutoka katika mikoa ya Dar es salaam, hasa maeneo ya Kinondoni, Tanga, Makete na Siha.
Mremi anasema “Utafiti wetu uliwahusisha
wasichana na wanawake wa rika kuanzia miaka 15 na kuendelea na kada
tofauti katika jamii kama wanafunzi, wafanyakazi, wahudumu wa bar,
wauguzi, makahaba na akina mama wa nyumbani
Katika maeneo hayo watu 903 walijitokeza wakiwepo pia wanaume ambao walihusishwa katika utafiti huo.
Imani potofu kwa wanaume
Wanaume waliohojiwa wamesema wanafanya kwa ajili
ya kupata raha tu na imani ya kuwa huko hakuna maaambukizi ya VVU, kitu
ambacho ni uongo, kwani huko ndiko kwenye kuchangia ukimwi kwa haraka
zaidi kuliko sehemu nyingine yoyote.
Katika
utafiti huo, wanawake 44 kati ya 166 waliohojiwa walisema wanafanya
tendo la kujamiiana kinyume na maumbile, licha ya kwamba ni jambo
linalokatazwa na dini zote.
Tanga yaongoza
“Tanga ndiyo kumeonesha kukithiri kwa vitendo vya
wanawake kufanya mapenzi kinyume na maumbile ukilinganisha na Makete
ambako bado kuna idadi ndogo” anasema Mremi
Fikra za kulinda ubikira
Ilibainika kuwa wasichana wengine walikiri kufanya
hivyo kwa ajili ya kulinda ubikira wao na baadhi ni mila na tamaduni za
baadhi ya makabila.
Dk Mremi amekaririwa akisema “ Utafiti wetu
uliwahusisha wasichana na wanawake wa rika kuanzia miaka 15 na kuendelea
na kada tofauti katika jamii kama wanafunzi, wafanyakazi, wahudumu wa
baa, wauguzi, makahaba na akina mama wa nyumbani. Katika maeneo hayo
watu 903 walijitokeza wakiwepo wanaume ambao walihusishwa katika utafiti
huo”.
Wakati wa utafiti huo wanawake 44 kati ya 166 waliohojiwa walisema wanafanya tendo hilo.
Dk Eliza Shayo, ambaye pia alishiriki katika
utafiti huo anasema sababu ya kufanya utafiti huo ilikuwa ni kuangalia
visababishi vya kusambaa kwa Ukimwi.
“Lakini pia tuliweza kujua tatizo la kufanya mapenzi kwa njia hiyo lina ukubwa kiasi gani” anasema
Dk Shayo pia anasema utafiti huo uliangalia iwapo
wanaofanya vitendo hivyo hutumia kondom au la. Wengi walionekana
kutotumia kondom wakifikiri hawawezi kupata virusi vya Ukimwi, imani
ambayo sio sahihi.
Ni changamoto
Mwenyekiti wa Mtandao wa Jinsia Kusini mwa Afrika,
(GEMSAT) Dominica Haule anasema utafiti huu ni changamoto kwa
serikali, watunga sera na vyombo vya sheria.
“Ni wakati muafaka wa kujadiliana nini kifanyike kupunguza tatizo hili. Hii ni hatari na haikubaliki,” anasema Haule
Anasema wadau wa afya hawana budi kuhakikisha wanafuatilia kwa ukaribu na kuweka wazi madhara ya vitendo hivyo.
Mhadhiri wa Masuala ya Saikolojia, Dk Kitila Mkumbo anasema suala hilo linaweza kuwa na athari kiafya.
“Kisaikolojia, kama wao wawili wamekubalina sawa, lakini kiafya lina athari kubwa,” anasema
Dk Mkumbo anasema ufanyaji wa mapenzi upo wa aina
nyingi wengine hufanyia mdomoni, inategemea na makubaliano, lakini
kiafya inaweza kuwa na athari.
Dk Meshack Shimwela, Daktari bingwa wa Magonjwa ya
Ndani ya Mwili kutoka hospitali ya Amana anasema mwanamke ambaye
hufanya mapenzi kinyume na maumbile huathirika na kuacha kufurahia tendo
hilo kwa njia ya kawaida.
“Lakini pia, wengi hujihisi kama wamelaaniwa na
wanakosa kujiamini” anasema na kuongeza kuwa hata kama anaweza kufanya
kwa mkumbo, baadae hujutia hasa anapojikuta anapata athari kubwa za
kiafya kuliko furaha.
Dk Shimwela anasema kitendo hicho husababisha bakteria wasiohitajika kuingia katika sehemu ya haja kubwa na kuleta uambukizo.
“Eneo la haja kubwa limeumbwa kutoa na si kuingiza. Hivyo kitendo hicho husababisha uharibifu na kulegea kwa misuli” anasema
Anasema maradhi mengine ambayo hujitokeza katika sehemu ya haja kubwa pindi mtu anapofanya mapenzi kwa njia hiyo hayana tiba.
Anaongeza kuwa wanawake hupata madhara wakati wa kujifungua na hatari ya kupata maambukizi ya VVU ni kubwa zaidi.
Jarida
la Havard la afya ya Wanawake (Havard Women Health Watch) linaeleza
kuwa ufanyaji wa mapenzi kwa njia ya haja kubwa ni chanzo kikuu cha
maradhi ya kuambukiza ukiwemo Ukimwi.Hii ina maana kuwa watu ambao
wanafanya vitendo hivyo wana athari kubwa za kupata virusi vya Ukimwi.
Kwanini ni hatari?
Tishu zilizo katika njia ya haja kubwa ni laini na
hazina maji maji, hivyo huchanika kwa urahisi wakati wa tendo na
kuingiza vijidudu.
Utafiti kama huu ulifanywa nchini Marekani mwaka 2005 na kituo cha Kudhibiti Maradhi ya Kuambukiza (CDCP).
Katika utafiti huo asilimia 40 ya wanaume na 35
ya wanawake wenye umri wa kuanzia miaka 25 na 44 walikiri kufanya tendo
hilo kinyume na maumbile.
Wanatumia matambala kuziba kinyesi
Kuna athari kubwa za kufanya kitendo hicho, baadhi
ya watu hujikuta wakivaa matambaza ili kuzuia kinyesi kisitoke kwa vile
mfumo wa haja kubwa huwa umelegezwa.
Profesa wa Chuo Kikuu cha tiba cha Colombia, Judy
Kuriansky anasema “Inashangaza kuona watu wanafanya mapenzi kwa njia
hiyo wakidhani wanajikinga na Ukimwi, huko ni kujidanganya, ukweli ni
kuwa njia hiyo ndio inayoweza kumfanya mtu kupata virusi kwa urahisi
zaidi”.
No comments:
Post a Comment