Thursday, May 2, 2013

LIPA MADENI UNAYODAIWA.

 
            LIPA MADENI                                    UNAYODAIWA.
1.    Warumi 13:8-10 . Deni lipi tulilonalo?
     -Deni kubwa tulilonalo ni upendo.
     “Msiwiwe na mtu cho chote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendae mwenzake ameitimiza sheria. Maana kule kusema, Usizini, Usiue, Usiibe, Usitamani; na ikiwapo amri nyingine yo yote, inajumlishwa katika neno hili, ya kwamba, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Pendo halimfanyii jirani neno baya; basi pendo ndilo utimilifu wa sheria”.

2.    Mathayo 22:36-37. Upendo unaoneshwaje?
     “Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu? Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote”.

3.    Yoeli 2: 15-16,17.
     -Watu wote wanatakiwa wamueshimu Mungu.
     “Pigeni tarumbeta katika sayuni, Takaseni saumu, kusanyeni kusanyiko kuu; Kusanyeni watu, litakaseni kusanyiko, Kusanyeni wazee, kusanyeni watoto, Na hao wanyonyao maziwa; Bwana arusi na atoke chumbani mwake, Na bibi arusi katika hema yake. Hao makuhani, wahudumu wa Bwana, na walie kati ya patakatifu na madhabahu, Na waseme, Uwaachilie watu wako, Ee Bwana, Wala usiutoe urithi wako upate aibu, hata mataifa watawale juu yao; Kwani waseme kati ya watu, Yuko wapi Mungu wao?”

4.    1 Timotheo 5:1
     Mzee usimkemee, bali umwonye kama baba; na vijana kama ndugu;”
     -Zama za mwalimu/ ujamaa mtoto alikuwa wa jamii yote lakini hivi sasa mtoto ni wa familia peke yake na imefikia hatua mtoto amekuwa ni wa mzazi mmoja ama baba au mama.
     -Mtoto asimami kwenye basi wakati mtu mzima au mzee anapoingia kwenye basi.
     -Mzazi wako akisha zeeka una wajibu wa kumtunza / kuwatunza.
     -Wazee hawafundishwi kwa maneno bali wanafundishwa kwa matendo hasa wale walio watelekeza watoto wao wakati wa ujana.

5.    Mithali 3:27-30
     “Usiwanyime watu mema yaliyo haki yao, Ikiwa katika uwezo wa mkono wako kuyatenda. Usimwambie jirani yako, Nenda, urudi halafu, na kesho nitakupa; Nawe unacho kitu kile karibu nawe. Usiwaze mabaya juu ya jirani yako, Ambaye ankaa karibu nawe na kujiona salama. Usishindane na mtu bila sababu, Ikiwa hakukudhuru kwa lolote.”
     -Watu wengine wanawazungusha majirani wenye shida. Kama unacho na kipo karibu mpe lakini kama hakipo mwambie hakipo kweli. Pia usishindane na watu bali lipa ubaya kwa wema.

6.    Mathayo 15:4-9.
    “Kwa kuwa Mungu alisema, Mheshimu baba yako na mama yako, na, Amtukanaye baba yake na mama yake kufa na afe. Bali ninyi husema, Atakayemwambia babaye au mamaye, Cho chote kikupasacho kusaidiwa na mimi ni wakfu, basiu asimheshimu baba yake au mama yake. Mkalitangua neno la Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu. Enyi wanafiki, ni vema alivyotabiri Isaya kwa habari zenu, akisema, Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami. Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu.”
     -Unapokataa kuwasaidia wazazi wako huku ukisema ninaenda kumwabudu Mungu wafanya kazi bure. Upendo ndio deni letu.

No comments:

Post a Comment