Mgonjwa huyu anahudumiwa kwa kupitia tiba ya mionzi hospitalini. Pamoja
na uzuri wake aina hiyo ya tiba ina athari kubwa kwa mwanadamu
isipotumiwa kwa usahihi. Picha kwa hisani ya mtandao wa
www.
kalenehospita
Na Joseph Zablon
Daktari huyo anatajwa kufariki kutokana na kansa ya
damu, na baadhi ya watu waliokuwa karibu nae kikazi, wakiwemo waliokuwa
wanafunzi wake, wanabainisha kuwa daktari huyo baadhi ya nyakati hakuwa
akivaa vifaa vya kumkinga na mionzi.
Daktari bingwa wa masuala ya mionzi katika
hospitali moja kubwa nchini aliyefariki miaka kadhaa iliyopita, kifo
chake kinahusishwa na athari za mionzi aliyokutana nayo kazini kwake
katika chumba cha X-Ray, hospitalini hapo.
Daktari huyo anatajwa kufariki kutokana na kansa
ya damu, na baadhi ya watu waliokuwa karibu nae kikazi, wakiwemo
waliokuwa wanafunzi wake, wanabainisha kuwa daktari huyo baadhi ya
nyakati hakuwa akivaa vifaa vya kumkinga na mionzi.
Ikiwa ni miaka kadhaa sasa tangu afariki, watoto
zake wawili aliowaacha wangali wadogo, nao wanasumbuliwa na kansa ya
damu na hata shule wanazosoma wamewekwa katika uangalizi maalum dhidi ya
watoto wenzao ambao ni watundu na wakorofi.
Daktari huyo ni mmoja kati ya maelfu ya watu ambao
wanapoteza maisha, kupata saratani na magonjwa mengine kutokana na
athari za mionzi iwe ya X-ray, T-scan au Utra sound ama kwa kukutana
nayo moja kwa moja au kutokana na kutumia huduma hizo mara kwa mara.
Kulingana na ripoti ya Kamati ya Wanasayansi ya
Shirika la Umoja wa Mataifa ya Kupambana na Athari za Mionzi ya Nguvu za
Atomic (UNSCEAR), tiba ya mionzi inachukua asilimia 98 ya vyanzo vyote
vya mionzi ulimwenguni.
Tiba hiyo ambayo ni pamoja na X-Ray, CT Scan, Utra
Sound na matumizi ya mionzi katika kutibu saratani, kwa kiwango
kikubwa ina madhara kwa binadamu na inaweza kusababisha kifo hasa kwa
mtumiaji wa mara kwa mara.
Ripoti hiyo inabainisha kuwa siku za karibuni
kumekuwa na ongezeko kubwa la matumizi ya mionzi katika tiba kuliko
wakati mwingine, huku ikikadiriwa kuwa zaidi ya vipimo bilioni 3.6 vya
X-Ray vinafanyika kila mwaka.
Mkufunzi wa mionzi katika Chuo cha Afya na Tiba
Muhimbili, Experditor Mahanja anasema mionzi inayotumika katika X-Ray,
Utra Sound, CT Scan ina athari kubwa inapokwenda moja kwa moja katika
mwili wa mtu ambaye sio mlengwa.
Anabainisha kuwa mionzi ina athari za kimaumbile
(Genetic) katika chembechembe hai katika mwili wa binadamu, na mtu
anaweza kupata saratani ambayo inaweza kuhama kutoka kizazi kimoja hadi
kingine, huku watoto wakizaliwa wakiwa na vilema na athari zingine.
"Hivi sasa sheria ni kali sana na udhibiti ni
mkubwa kulingana na sheria za kimataifa" anasema na kuongeza kuwa
kutokana na hali hiyo ndio maana kuna vizuizi maalum ambavyo vinatumika
kwa wafanyakazi walio katika vyumba vya X-Ray ili kuwakinga na mionzi.
Anasema kila baada ya mwezi, vizuizi hivyo
((Throming Detector),husafirishwa hadi katika Kituo cha Tume ya Nguvu za
Atomiki (IAEA) kilichopo Arusha kwa ajili ya ukaguzi wa kiwango cha
mionzi ambayo ipo katika vizuizi hivyo.
“ Kila baada ya mwezi kuna kiasi cha mionzi
ambacho kinatarajiwa kukutwa katika kizuizi hicho, na ikitokea dozi
ikazidi mtumiaji inabidi atoe maelezo au kuondolewa katika utendaji
kwani anakuwa hatarini" anasema.
Mahanja anatoa mfano wa mfanyakazi
mwenzao mmoja ambaye kifaa chake kilikutwa na kiasi kikubwa cha mionzi
kuliko kawaida baada ya kupelekwa kukaguliwa, hivyo alitakiwa kutoa
maelezo.
“Sheria ni kali za usimamizi wa matumizi ya mionzi
hivi sasa, na kutokana na kuongezeka kwa teknolojia athari za mionzi
zimethibitiwa kwa kiasi kikubwa kwa watumiaji hivi sasa kuliko wakati
mwingine” anaeleza.
Naye mwanasayansi mwandamizi katika Tume ya Nguvu
za Atomiki (TAEC), Dk. Wilbroad Muhogora anasema kupiga X-ray au kutumia
aina nyingine ya mionzi, inapaswa kuwa jambo la mwisho kufanywa kwa
mgonjwa kutokana na ukweli kuwa nishati hiyo sio rafiki kwa mwili wa
binadamu.
Anasema athari za mionzi zipo wazi na hata jumuia
ya kimataifa hulazimika kutoa uangalizi wa kipekee katika matumizi ya
minururisho hiyo.
Anaeleza zaidi kuwa mfano rahisi wa athari ni
mabomu ya nyuklia yaliyopigwa katika miji ya Hiroshima na Nagasaki
nchini Japani wakati wa mwisho wa Vita ya Pili ya Dunia Agosti 1945.
Dk Muhogora anasema athari za mionzi hiyo ya
nyuklia zinatajwa hadi hivi sasa, kwani watu wengi bado wanazaliwa
wakiwa na vilema, saratani za aina mbalimbali, kansa ya damu na athari
zingine ambazo zinasababisha magonjwa ya kurithi na hata vifo.
Anasema bado matukio ya athari za mionzi kwa
binadamu yapo mengi, na hata kuvuja kwa vinu vya nyuklia katika nchi za
Urusi Japani, ni ishara za wazi kuwa mionzi ingawa ina faida, lakini
pia ina athari mbaya kuliko inayofikiriwa.
"Mionzi katika maeneo hayo sio tu imeathiri
binadamu bali pia hata mimea, na ndio maana Serikali kupitia tume ya
mionzi ilitoa tahadhari kwa umma kuhusiana na vyakula vinavyotoka nje
hususan nchini Japan baada ya tukio la Fukushima" anasema.
Daktari wa saratani katika Hospitali ya Ocean Road
ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa kuwa si msemaji wa hospitali
hiyo, anasema elimu zaidi inahitajika hususan katika hospitali za ngazi
ya wilaya, kwani vifaa vya kujikinga ni vichache na havikidhi haja.
"Utakuta katika hospitali ya wilaya kuna
wafanyakazi wa X-ray watatu hadi wanne, lakini kifaa ni kimoja" anasema
na kuongeza kuwa hali hiyo inahatarisha usalama kwa wale wasiovaa kifaa
hicho wakati wa kazi.
Anaiomba serikali kuchukua hatu za makusudi
kuhakikisha vyumba vya mionzi au X-ray vinapata vifaa vya kutosha,
badala ya kuwa kama ilivyo sasa hususan katika hospitali za pembezoni.
No comments:
Post a Comment