TUNZA FAMILIA KWA KULIKABILI TATIZO LA VIJANA KABLA YA NDOA.
Siku
hizi kuna mvurugiko, ufisadi mpya, mkandamizo wa jamii, kutoa mimba na magonjwa
ya zinaa tele tele.
Baba
Fulani alishangaa kuona mabadiliko ya ya ghafla kwa binti yakeambaye alikuwa
mchangamfu/mzungumzaji, sasa mwenye wasi wasi, pita pita nyingi huku akiwa
amenuna. Hatimaye binti aliungama kuwa kijana wa kiume alimsihi kushirikiana
naye kimwili(ngono).Baba yake alisema: “Nilijua kuwa mabinti wengine………….
Lakini siyo kwa binti yangu!” Kosa liko
wapi?
Kilio
hiki sasa kimewakumba wazazi wengi, mivuto ya ufisadi mpya imekaribisha mauti
kwa vijana. Tunawezaje kuwasaidia vijana ambao wanazama katika bahari yenye
mawimbi makubwa ya ufisadi kote duniani. Ebu soma Yeremia 25:32, Mathayo
24:38-39, Mwanzo 6:5.
Tuwasaidieje vijana wetu?
1.Tudumishe
matengenezo kwa kumuitikia Mungu na kujali wajibu wetu, maana siku hizi watu
wapo bize katika kutafuta fedha na kusahau kuwapatia malezi bora watoto wao.
Ebu soma Malaki 4:5,6. Methali 22:6, Mwanzo 18:19.
Tuwaandae
watoto mapema sawa na kocha na wanariadha wake, tujiwekee program kabambe ya
kuwaelimisha na umri wao, na wafundishwe kanuni za wanariadha wa kiroho mapema.
2 Timotheo 2:4,5; 1 Wakorintho 9:24,25.
-Kuza uhusiano wao na
Mungu kwa mfano wako pia, yaani waone mfano wa mahusiano yako wewe mzazi na
Mungu wako kwanza.
-Tuthamini neno la
Mungu lisilokosea. Wafikie wakiwa bado kuvamiwa na dunia na falsafa za
kupotosha.
-Wafanye watambue
mahali wanapoweza kupata uwezo wa kushinda majaribu. Zaburi 119:9.
-Walinde vijana wako
kwa bidii isiyokoma.
-Usimwachie mtu
mwingine kazi hiyo, ifanye wewe mwenyewe.
-Usiwaachie majirani
kumlea mtoto wako. Kutayarisha njia ukurasa wa 163-165.
Tunapaswa kufanya
uchaguzi kati ya kupata vyote vya dunia hii na kukoswa watoto.
Hakuna mtu wa mbadala
ya Baba/mama. Mafunzo hayo maalumu yalenge mathalani mkandamizo wa jamii,
Mabadiliko ya ujinsia na majaribu yake.
Vile vile jibu
maswali yao kwa busara bila kudanganya, Usiwaachie tu waalimu wa biolojia
Shuleni, Waalimu wa mitaani wasimbabaishe.
Akiyakosa hayo
kutatokea nini? Mathayo 5:20-22,27; Mithali 5:23; 22:8 Waeleze hadithi yote na
matokeo yake.
2.Dumisha
wajibu uliopewa na Mungu wa Uongozi, Usiwaache wajiongoze wenyewe, Usiwe
hafifu, Chekibobu. Eleza thamani ya zawadi ya uanariadha 1 Wakorintho 9:22-27 Uzima wa milele. Panua
njozi zao za maisha ya baadae, Uwezo wa kuona kwa imani Waebrania 11:6, Zaburi
19:9-11 Waeleze juu ya ahadi za Mungu duniani na nchi mpya. Afya/kujibiwa
sala/ndoa n.k . Waebrania 13:4, Warumi 1:8
3.Wasaidie
kumtafuta Mungu wao wenyewe. Walete kwa Yesu mapema Mathayo 19:13-15. Watie
moyo kujifunza biblia, wafundishe kuomba. OMBA
NAO.
4.Watie
moyo kutembea na marafiki wazuri na wakweli. Dunia yasema “Play safe” tumia mipira
neno la Mungu jaribu tabia ”USIZINI”
MADARASA YAFUNDISHAYO UJINSIA BILA KUTHAMINI LISEMAVYO NENO LA MUNGU NI HATARI.
Methali 13:20; 1 Wakorintho 15:33. Kutayarisha njia ukurasa 181. Zaburi 1:1-2.
5.Wape
watoto shughuli za kufanya wasikae kizembe kizembe.Msemo wa zamani: “Shetani
hutafuta kuitumia mikono isiyo na kazi” Watie moyo kushiriki mazoezi ya viungo.
6.Wape
wajibu wa kufanya na uone namna wanavyoendelea. Wafundishe kazi za kujitegemea
mfano Bustani n.k . Uwe kando ukiwasaidia, ukiwatia moyo kuendelea mbele,
Wasikilize, Gundua wanayopendezwa watie moyo wanapofanikiwa.
7.Wapatie
maburudisho yafaayo, weka katika maktaba vitabu vinavyofaa. Waelezee faida na
hasara ya vitabu vizuri na vibaya.
No comments:
Post a Comment