Tuesday, September 3, 2013

WAUAJI WAKATILI




WAUAJI WAKATILI
“Mikono yako ilinifanya ikanitengeneza , unifahamishe ukanifahamishe nikajifunze maagizo yako” (Zaburi 119:73.)
            Kiasi ni matokeo ya kujitawala,pia kiasi inatusaidia kuweka mipaka kwa vitu fulani na pia kutotenda kabisa vitu vingine.Tukirejea katika fungu letu hapo juu la Zaburi 119:73 utaona mtunga Zaburi akimwuliza Mungu ampatie ufahamu.Ufahamu utakaomwezesha Daudi kujifunza sheria za Mungu.

Sisi pia twaweza kumwomba Mungu kuhusu afya zetu ili atusaidie kutii sheria kuhusu kiasi.Mungu alituumba hivyo anafahamu lililojema kwetu kimwili,kiakili,na kiroho.
KUFANYA KUPITA KIASI
            Soma mafungu yafuatayo:- Mithali 20:13; Mhubiri 3:17; Mhubiri 12:12;       Marko 4:19.
Zingatia jinsi kujitawala kunavyoelezewa labda utashangaa.
1.”Kula, Kunywa au kulala kupita kiasi ni dhambi. Mwili na akili yenye afya huleta furaha.”(Temperance, uk.138)
2.”Lazima tuwe na kiasi kazini mwetu.....
”Kazi ya siku isiendelee hadi usiku....Mungu amenionyesha kuwa watu ambaohuendelea na kazi kwa muda mrefu sana hupoteza zaidi kuliko kufaidi. Huunguza nguvu zao, na huendelea kutenda kazi wakitumia msituko wa Neva (nervous excitement).” (Temperance,uk.139,140).
3.”Kujifunza kwa muda mrefu ni sawa na kunywa kupita kiasi. Watu wajifunzao kupita kiasi watakuwa na matatizo.” (Temperance, uk.140).
4.”Sababu mojawapo ya afya mbovu kwa wanaume ni tamaa yao kuu kutaka wapate fedha . Kusudi mahsusi kwa baadhi ya wanaume ni kupata fedha. Wanjinyima pumziko, usingizi, na kila burudani nzuri maishani, ili kupata utajiri.” (Temperance, uk. 140).

Watu wenye kupenda fedha wanafanyaje wanaposikia ujumbe wa injili? Marko 4:19.
Watu watajwao katika Luka 12:16-21 na Luka 18:18-23 walikuwaje? Tamaa ya fedha ilitawalaje maisha yao? Habari zao hutusaidiaje kuelewa Marko 4:19?
            Wote wawili walifurahi kupata fedha kiasi kwamba walipuuza hazina kubwa mno yaani uzima wa milelepamoja na Mwokozi. Kutokuwa na kiasi kuliifungia nje injili isipenye mioyoni mwao na pia kuwazuia kujenga tabia za kimbingu.

           


KULA KUPITA KIASI (Mithali 23:1,2,21).
Ni dhambi gani ya kawaida leo?
”Ulafi ni dhambi iliyoenea sana siku hizi. Tamaa mbaya ya chakula hufanya wanaume kwa wanawake kuwa watumwa. Kula kupita kiasi huzuia mtu kufikiri vizuri hivyo kumfanya asiweze kufurahia ukweli wa neno la Mungu.” (Testimonies, Vol. 1, uk. 486).
            Ulafi sio kutumia kujitawala. Tunahitaji akili timamu ili kuelewa mapenzi ya Mungu katika maisha yetu. Ulafi huathiri nguvu joto za watu kuliko kufanya kazi kupindukia. Chakula kisicho hitajika huziba mishipa kwa sababu hakiwezi kutengenezwa nyama au damu. Chakula kisichotumika ni mzigo kwa ini na hudhoofisha mwili. Counsel on Diet uk.102,103.

Ni ushauri gani tuupatao kutoka katika Mithali 23:1,2,21? Je mlafi awezaje kuwa maskini?
            Mithali 23:2 haisemi ujiue iwapo u mlafi; bali hushauri umuhimu wa kujitawala. Mtunzi wa Mithali husisitizia kuwa kula kupita kiasi ni tatizo baya, lazima tuwe waangalifu sana.

            AKILI HAFIFU; MADAWA YA KILA SIKU (Mithali 25:27; 1 Korintho 10:31).
Mithali 25:27 husema haifai kula asali nyingi mno.Je ni neno gani la kisasa ambalo tungeweza kulitumia badala ya neno ”asali”?
Akili hafifu:Sukari husababisha chachu,na hii huifanya akili iwe hafifu na mtu aharibikiwe. ”Mungu amenionyesha kuwa kiasi kikubwa cha sukari kina madhara makubwa kuliko nyama.” (Counsels on Diet and Foods, uk 327,328).
Sukari nyingi mno huwa ni chanzo cha matatizo mengi ya kiafya. Utumiaji wa sukari nyingi huleta matatizo katika uozaji wa meno. Sukari nyingi  ( na mafuta mengi) huweza kuleta tatizo la ”uzito mkubwa”.Kufa katika umri mdogo huongezeka kadri unene unavyozidi mno.
Upo uhusiano pia kati ya sukari na ugonjwa wa kisukari. Mtu mwenye uwezekano wa kupata ugonjwa wa kisukari aweza kuchelewa kupata ugonjwa huo kwa kutumia chakula chenye wanga tele(nafaka isiyokobolewa) na sukari kidogo.
Na mwisho, sukari hudhoofisha chembechembe nyeupe za damu. Chembechembe hizo ni muhimu kwa kuuwezesha mwili kupambana na magonjwa na vijidudu vya maradhi.

Vileo vya kila siku: Je, kahawa, chai, baadhi ya madawa ya kupunguza maumivu na vinywaji baridi; vyote kwa pamoja vimejaa nini?
Vyote kwa pamoja vimejaa Kafein. Kafein ni dawa ya kulevya, hivyo itasababisha matatizo ya kiafya. Kafein huleta ongezeko la sukari katika damu, ongezeko la msukumo wa damu, na ongezeko la mapigo ya moyo. Kafein yaweza kusababisha vidonda vya tumbo, na magonjwa ya moyo.
            Kafein yaweza kumfanya mtu awe mchangamfu sana au mnyonge aliyezubaa ajabu. Pia Kafein huweza kuleta madhara kwa viumbe ambavyo havijazaliwa. Majaribio yaliyofanywa katika wanyama  huonyesha kuwa Kafein nyingi husababisha viumbe vichanga kuzaliwa vyenye mifupa dhaifu, kuzaliwa na uzito pungufu, au kuzaliwa vimekufa.
            Madhara ya Kafein huonekana kwa kutumia tu kikombe kimoja hadi vitatu vya kahawa. Mtoto ndogo atumiapo chupa moja tu ya soda yenye kKafein hupata madhara sawa na mtu mzima aliyetumia vikombe vinne.

Ebu tafakari baada ya kusoma 1 Korintho 10:31.Je kafein au sukari nyingi yaweza kuwa kikwazo katika ufahamu wako wa mambo ya kiroho?

            NI NANI ALIYE NA MACHO MEKUNDU?” (Mithali 23:29-35)
Ni nini katika nchi zinazoendelea na zilizoendelea kilicho chanzo cha asilimia 30 za wanaojinyonga; chanzo cha asilimia 55 za  ajali za barabarani; Chanzo cha zaidi ya asilimia 60 za mateso kwa watoto; na chanzo cha asilimia zaidi ya 80 ya ujambazi wote? Mithali 23:29-35. (Takwimu kutoka Kathleen Whalen Fitzgerald,Alcoholism, [New York:Doubleday, 1988],uk. Xii).
Chupa moja au mbili tu za pombe hufanya ubongo usiweze kukusanya habari toka katika vitu viwili tofauti. Kiasi hicho cha pombe hupunguza kukumbukumbu, kuona, ufahamu, na maamuzi. Pia huathiri utaratibu wa mwili; kwa mfano:
1.Mfumo wa kinga: Pombe hupunguza uwezo wa chembechembe nyeupe za damu kuweza kupambana na maradhi. Pombe huongeza uwezekano wa kuugua kichomi, kifua kikuu, homa ya manjano, na kansa mbalimbali.
2.Mfumo wa misisimko muhimu mwilini (Endocrine system): Chupa mbili au tatu tu kwa siku huongeza uwezekano wa kutoka mimba, kuzaa motto aliyekufa, au kuzaa mtoto asiyekomaa.
[Mfumo huu unayo viungo muhimu (glands) ambavyo hutengeneza dawa maalumu (homones) ambazo husafirishwa na damu kwenda zinakohitajika mwilini kusisimua utekelezaji wa kazi muhimu mwilini. Kwa mfano Pancreas Gland (kongosho) hutoa dawa iitwayo Insulinambayo husisimua kazi ya uyeyushaji wa wanga kuwa sukarirahisiifaayo kutumika mwilini. Pia ipo Gland inayotoa madawa ya kusisimua kazi za uzazi mwilini; na kwa wanawake gland hiyo (ovary) hutoa madawa ya Progesterone na Esterogen ambayo husisimua matendo yanayohusika ili mama mjamzito apate kujifungua ipasavyo. Ulevi hudhuru taratibu za mfumo huu.]
3.Mfumo wa mzunguko wa damu: Kutumia pombe huongeza uwezekano wa ugonjwa wa moyo na hupunguza uwezekano wa ugonjwa wa moyo na hupunguza kiasi cha sukari kihitajikacho damuni. Pombe huongeza mafuta damuni na kuleta tatizo la msukumo mkali wa damu.
4.Mfumo wa usagaji wa chakula: Pombe huvuruga tumbo na kusababisha vidonda vya tumbo. Na sehemu idhuriwayo mno na pombe ni ini.
(Ini ni kiungo muhimu sana kwani huhusika kuharibu sumu au vijidudu vibaya vivamiavyo mwili. Basi utumiapo kwa hiari vinywaji vikali, unaongeza sumu na ini linapambana nazo, na lishindwapo kuzimudu lenyewe hudhurika. Na baada tu ya muda wa masaa 8 hadi 24 baada ya ini kukoma kumudu shughuli zake mtu hufa.
Mungu ameumba ini kwamba iwapo ni sumu kidogo imelidhuru, basi ini linao uwezo kuunda chembechembe mpya kujijenga upya, ila sumu iwapo imlivuruga lote, hasa kwa pombe kali, basi linakwama kwa kudhuriwa na sumu kali, na mhusika huaga dunia).

Mambo ya Walawi 10:1-11 huthibitishaje kuwa kileo hudhuru uwezo wa mtu wa kufanya uamuzi?
            Pombe na vileo vikali hudhuru ubongo kiasi kwamba watu hushindwa kutofautisha kati ya lililo sahihi na lililo kosa. Hawawezi kutofautisha kati ya lililo takatifu na lililo ovu; lililo safi na lililo najisi.
            “Kutumia vileo kuliwafanya wale wana wawili wa Haruni. Nadabu na Abihu, wachukue moto wa kawaida walipoingia katika hema ya kukutania. Vijana hawa hawakuijua tofauti iliyokuwepo kwani walikuwa wamelewa.” (SDABC,Vol.1, uk. 749).

           



LAKINI IMEANDIKWA KATIKA BIBLIA(Kumbukumbu la Torati 14:22-26, 1Tmotheo 5:23).
            Leo tunajifunza mafungu ya Biblia ambayo Wakristo huyatumia kuhakikisha kuwa kutumia kileo kidogo si dhambi.
            Neno ”divai” lilitumika kwa Waebrania kuwakilisha kinywaji kitokanacho na zabibu zilizokamuliwa. Walitumia neno ”yayin”.
            Kinywaji hiki hakikuwa kileo. Lakini kilipoachwa kwa muda mrefu kilichacha na kuwa kileo. (tukumbuke Agano la kale liliandikwa kwa Kiebrania).
            Katika agano jipya neno ”divai” limetokana na neno la kiyunani,  ”oinos”. Ukumbuke kuwa Agano jipya lugha yake ya awali ni Kiyunani). Hapa pia ”oinos” imetumika kuwakilisha kinywaji kitokanacho na zabibu zilizokamuliwa. Usomapo Yohana 2:1-10
            Yesu aliwanywesha watu katika harusi ya Kana ya Galilaya kinywaji safi, kitamu, kisicholevya. Kimetajwa kuwa ni ”divai”.
            Kumbukumbu la Torati 14:22-26 huelezea jinsi makuhani walivyokuwa wanawaelekeza wana wa Israeli kuandaa sikukuu ya mwaka ya mavuno wakati waletapo zaka kwa Mungu kushukuruwema wake. Je unadhani kinywaji kilichotumika hapa ni pombe? La hasha, watu wa Mungu hawangekuwa wanapokea rasmi mafundisho nyeti ya kiroho wakiwa wamelewa.

            Katika 1 Timotheo 5:23 Paulo anampatia Timotheo ushauri kuwa atumie mvinyo kidogo kwa ajili ya tumbo lake. Neno la kiyunani lililotumika pale ni ”oinos”. Neno lenye maana ya kinywaji kilichotokana na kukamua zabibu. Swali litakuwa kama kinywaji hicho kilikuwa safi au kiliachwa hadi kikachacha kiwe kileo?

            Historia hueleza kuwa divai isiyochacha, kinywaji safi cha mizabibu, kilitumika kama dawa. Aristotle(384-322BC), Pliny(AD 24-79; mtu aliyeishi wakati mmoja na Paulo), na Athenaeus(AD 280); kila mmoja wao kwa wakati wake huzungumzia matumizi ya kinywaji safi cha mizabibu, yaani divai isiyochacha, kama dawa nzurikwa matatizo ya tumbo.
            Kumbuka: Aliambiwa asitumie maji tu bali mvinyo kidogo. Wengine leo huchukulia kama aliambiwa  ”usitumie divai tamu ila tumia pombe kwa ajili ya tumbo lako.”  Je ushauri wa Paulo katika  1 Timotheo 6:11,12 ungekuwa wa busara gani iwapo kweli alikuwa anamshauri Timotheo kutumia pombe kama dawa?  (Kwa maelezo zaidi, soma ”Wine in the Bible” kilichoandikwa na Samuele Bacchiocchi, na kucahapishwa na Biblical Perspectives, 4569 Lisa lane, Barren Springs, Michigan 49103).






NI MAGONJWA GANI YATOKANAYO NA UVUTAJI WA TUMBAKU?
Tumbaku hudhuru kila sehemu ya mwili wa binadamu ambamo hugusa. Tangu kansa ya ulimi, mdomo, mapafu, moyo, tumbo, ni muuaji namba moja. Tumbaku haisababishi kulewa, ila inayo sumu kaliiitwayo ”Nikotini”. Nikotini huathiri ubongoni katika kipindi cha sekunde saba. Hii ni mara mbili haraka zaidi kuliko muda utumiwao na sumu ya sindano ya madawa ya kulevya (Heroin).
            Biblia haiitaji tumbaku kwa vile ilikuwa haioteshwi katika nyakati za Biblia. Unafikiri ni mafungu yapi katika Biblia hutuagiza kuachana na uvutaji?
            Ebu soma Ufunuo 22:14,15 angalia neno ”wachawi”. Neno la kiyunani lililotumika hapa ni ”pharmakos”likimaanisha  ”alishaye wengine sumu”. Neno linalofanana na hilo ni  ”pharmakon” linalomaanisha ”madawa ya kulevya”. Wachawi wa kale walitumia madawa ya kalekulevya; na na iliandikwa katika Ufunuo 22:15 kuwa watakuwa nje ya jiji la Yerusalemu mpya. Je watu leo wasisitizao matumizi ya madawa ya kulevya(wachawi wa leo) hukumu yao itakuwaje mbele za Mungu?
           

HITIMISHO:Mungu alituumba, kwa hiyo tunaweza kumwomba atusaidi kufahamu kanuni zake za afya.Halafu tuzitumie kanuni hizi katika maisha yetu ili tuweze kuwa na dhamira safi kufahamu na kutenda mapenzi ya Mungu.

REJEA:
Ellen G White,Counsels on Health, uk. 71,157,160(kuhusu ulafi); uk 81-90 
            (kuhusu tumbaku na madawa ya kulevya);uk. 98-100 (kuhusu kutumia kadri tu na
            Kiasi).
Ellen G White,Christ’s Object Lessons, Faida ambayo ni Hasara, uk.252-259.
Ellen G White, The Desire of Ages, Umepunguk            Sisi pia twaweza kumwomba Mungu kuhusu afya zetu ili atusaidie kutii sheria kuhusu kiasi.Mungu alituumba hivyo anafahamu lililojema kwetu kimwili,kiakili,na kiroho.


No comments:

Post a Comment